Tafadhali angalia FAQ ili kuona kama swali lako tayari limejibiwa. Ikihitajika unaweza kuwasiliana nasi na tutafanya tuwezavyo ili kuwasiliana nawe haraka iwezekanavyo, lakini tuwie radhi kwani sisi ni timu ndogo na kwa hivyo tunakuomba utufahamu.
Kwa bahati mbaya, hapana. Hatutoi utendaji wa kupakua tovuti yetu au Qur'ani kwenye kompyuta yako kwa sasa. Hata hivyo, unaweza kusakinisha programu yetu ya simu kwa usomaji wa nje ya mtandao.
Ili kubadilisha lugha unayopendelea, kuna menyu kunjuzi kwenye kona ya juu kulia kwenye kila ukurasa (kona ya juu kushoto kwenye lugha za kuandikwa kutoka kulia kwenda kushoto). Tumia menyu kunjuzi hii kuchagua lugha unayopendelea.
Tafadhali ripoti hitilafu hii hapa na tutairekebisha kwa haraka iwezekanavyo inshAllah.
Hiyo si nzuri! Ikiwa tovuti haifanyi kazi kabisa au labda unaona skrini nyeupe yenye maandishi 'Samahani, hitilafu imetokea', tutashukuru ikiwa unaweza kuripoti hapa .
Tafadhali angalia ukurasa wa wasanidi kwa maelezo zaidi.
Quran.com ni zana ya kusoma, kusikiliza na kufanya uchunguzi mtandaoni. Timu iliyo nyuma ya Quran.com inajumuishwa na wahandisi wa programu, wabunifu na meneja wasimamizi. Kwa bahati mbaya, huu ndio ukomo wa ujuzi wetu. hatuna wanazuoni, maimamu au masheikh wanaoweza kusaidia kujibu maswali ya Kiislamu, Fiqh au kupeana Fatwa. Tunajaribu kujizuia kujibu lolote kati ya maswali hayo na kukushauri uzungumze na imamu wako au sheikh msikitini karibu nawe.
Ndiyo, tunazo baadhi ya Tafsir. Bofya kwenye ikoni iliyoonyeshwa kando ya kila aya, kisha ubofye tafisr. Programu itakuonyesha orodha ya tafsir zinazopatikana. Bonyeza tafsir unayotaka kusoma.
Fungua toleo jipya hapa lenye maelezo yote, kiungo cha tarjuma na tutajaribu tuwezavyo kuliongeza.
Wasilisha maelezo zaidi kuhusu msomaji huyu hapa
Ndiyo! Tafadhali tembelea ukurasa wetu wa programu za simu kwa maelezo zaidi.
0%