Kutuhusu

Quran.com ilianzishwa mwaka 1995. Tovuti hii inalenga kumrahisishia mtu yeyote kusoma, kuchunguza na kujifunza Qur'ani. Mradi huu ni open source na umeundwa kupitia ushirikiano kati ya washiriki wakuu na timu ya Tarteel.

Utambuzi

Mradi huu haungewezekana bila maktaba nyingi ya open source na miradi ambayo tumetumia:

  • Tanzil: Mradi wa kimataifa wa Qur'ani unaolenga kutoa maandishi sahihi ya Qur'ani yaliyothibitishwa.
  • QuranComplex: King Fahd Glorious Qur'an Printing Complex ni kiongozi katika kuitumikia Qur'ani Tukufu na Sayansi zake, kutafsiri Maana zake, na kuyalinda Maandishi ya Qur'ani yasipotoshwe, kwa matumizi bora ya teknolojia za hali ya juu katika uwanja wa uchapishaji, rekodi za sauti, uchapishaji wa kielektroniki na matumizi ya kidijitali.
  • Collin Fair: Chombo cha kutengeneza maneno sahihi ya usomaji wa Qur'ani yaliyorekodiwa.
  • QuranEnc: Tovuti yenye tarjuma za bure na za kuaminika za maana na ufafanuzi (Tafsir) wa Qur'ani tukufu katika lugha nyingi za ulimwengu.
  • Zekr: Jukwaa la jamii la kujifunza Qur'ani kwa ajili ya kuvinjari na kutafiti juu ya Qur'ani
  • Lokalize: Mfumo wa tarjuma wa kidijitali unaoangazia tija na uhakikisho wa ubora na hutoa mtiririko wa kazi wa ujanibishaji.
    Lokalise
  • Vercel: ni jukwaa la uwekaji na ushirikiano kwa wasanidi programu wa mbele ambalo huweka msanidi programu kwanza, na kuwapa zana za kina za kuunda tovuti na programu zenye utendakazi wa hali ya juu.
    Vercel

Ongeza matumizi yako ya Quran.com hadi upeo!
Anza ziara yako sasa:

0%